Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Taarifa kwa vyombo vya habari
Taarifa kwa vyombo vya habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 28 Novemba, 2017 amewasili Mjini Nairobi nchini Kenya ambako anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba amepokelewa na Mhe. Balozi Robinson Njeru Githae wa Kenya na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. Pindi Chana.

Sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta zinafanyika katika uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Nairobi

28 Novemba, 2017