Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

taarifa kwa vyombo vya habari
taarifa kwa vyombo vya habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Tarehe 07 Septemba, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na kamati maalum mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai.

Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hafla ya kukabidhiwa kwa taarifa hiyo itarushwa moja kwa moja na vituo vya redio na televisheni kuanzia saa 4:00 Asubuhi.

Wananchi wote mnaombwa kufuatilia matangazo hayo kupitia vyombo vya habari na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

06 Septemba, 2017