Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

taarifa kwa vyombo vya habari
taarifa kwa vyombo vya habari

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu : +255-22-2114512, 2116898

Email : press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz

Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM,

TANZANIA


Rais  wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar esSalaam  amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof.Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  (TRA) ilikutoa uelekeo wa Serikali anayoita kamara baada ya kuapishwa.

“Nataka Serikalii endelee kwanguvu zote na katika kutekeleza dhana ya‘HAPA KAZI TU’naviongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.

Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa nilazima kilamtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.

Katika kikao hicho Rais  ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapoteua Baraza lake la Mawaziri  mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakao teuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.

Mambo  hayo muhimu ni kamaifuatavyo:

Kuanzia mwezi Januari  mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwautekelezaji

Suala la mikopo yawanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi

Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapo litole asuala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchizifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania  wanao wakilisha nchi huko nje.

 

Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu  Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianzekutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.

Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa  mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wakuto amaamuz ivinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais ama Makamu wake.

Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, nakuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria  na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema yakazi.

 

………………………MWISHO……………………

Imetolewa na  Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

7 Novemba, 2015 .