Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Bunge

Baraza la Kutunga Sheria au Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. Rais anatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba kwa kuridhia miswada ya sheria ya bunge ili kukamilisha mchakato wa kutunga sheria kabla ya kuwa sheria.

Sehemu hii inakupa taarifa kamili kuhusu bunge ambalo ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kina madaraka kwa niaba ya wananchi, kusimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Bunge lina aina nne za wabunge, yaani:Wabunge waliochaguliwa moja kwa moja kuwakilisha majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar;Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe, Mwanasheria Mkuu;Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais na wabunge wanawake wasiopungua 15% ya makundi mengine yote kwa msingi wa uwiano wa uwakilishi miongoni mwa vyama vilivyomo katika Bunge. Kwa taarifa zaidi tembelea  Bunge la Tanzania

 

Bunge la Tanzania lina makundi ya wabunge yafuatayo: (Rejea Ibara ya 66 ya Katiba).Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo yao.Wabunge wanawake ambao idadi yao itaongezeka hatua kwa hatua kuanzia asilimia ishirini ya wabunge kama ilivyotajwa katika aya ndogo ya (1), (3) na (4) ya aya hii, Watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa bungeni kwa mujibu wa Ibara ya 78 ya Katiba na kwa msingi wa uwiano wa idadi ya wabunge miongoni mwa vyama. Wabunge wa tano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wao, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, si zaidi ya wabunge kumi walioteuliwa na Rais.

Katika kutekeleza kazi zake, Bunge linasaidiwa na Tume ya Huduma za Bunge, Kamati za Kudumu na Sekretarieti ya Bunge. Kazi kuu za Bunge ni: 1) Kumhoji waziri yeyote kuhusu masuala ya umma yaliyo ndani ya dhamana yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; 2) Kujadili utendaji wa kila wizara wakati wa kikao cha mwaka cha Bunge la bajeti; 3)Kujadili na kuidhinisha mpango wowote wa muda mrefu au mfupi unaotakiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; 4)Kutunga Sheria pale ambapo utekelezaji unahitaji sheria na; 5) Kujadili na kuridhia mikataba na makubaliano ambayo Jamhuri ya Muungano ni mhusika na masharti yake yanahitaji idhini.

Aidha hutunga sheria zinazotumika kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia Bunge hutunga sheria zinazotumika Tanzania Bara tu; Zanzibar ina Baraza la Wawakilishi wake linalotunga sheria mahususi kwa Zanzibar (Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lina wajumbe 50, wanaochaguliwa kutumikia kwa kipindi cha miaka mitano).