Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovuti Rasmi ya Rais
Ofisi ya Rais - Ikulu

Mahakama

Mahakama nchini Tanzania ina vyombo vitatu: Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahakama Kuu za Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa Tanzania Bara. Mahakama za Hakimu Mkazi na Mahakama za Mwanzo.

Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa Tanzania Bara ina:Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania(Mwenyekiti); Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania; Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu; na Wajumbe wawili walioteuliwa na Rais.

Mfumo wa sheria ya nchini Tanznaia unaongozwa na Jaji Mkuu na Msajili wa Mahakama ya Rufaa kama Mtendaji Mkuu. Jaji Kiongozi(JK) akisaidiwa na msajili wa Mahakam Kuu, ndiye anayesimamia utawala wa Mahakama Kuu na Mahakama zilizo chini yake.

Mahakama Kuu imegawanyika katika Kanda, zinazosimamiwa na Mahakimu wafawidhi wakisaidiwa na Wasajili wa Wilaya.Katika ngazi za Wilaya na Mkoa, utawala uko chini ya Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mkoa na Wilaya. Mahakimi Wafauidhi wa Wilaya pia wanasimamia Mahakama za mwanzo katika wilaya zao zinazohusika.

Kutoka kwenye uchumi dhabiti kuelekea kwenye ufunuo wa soko huria nchini Tanzania, kumeifanya Mahakama ikabiliane na hukumu tata katika maeneo kama sheria ya ushirika, sheria ya kazi na ubunifu, sheria ya biashara, miamala ya biashara ya kimataifa, miamala ya ardhiuhalifu wa kimataifa, udanganyifu katika miamala ya fedha ya kimataifa na aina nyingine za uhalifu wa kiofisini. Haili hii inahitaji utaalamu na ubobezi zaidi, hasa katika sheria za biashara. Tanzania kama zilivyo mamlaka nyingine za sheria, imeshughulikia tatizo hili kwa kuamua kuanzisha kitengo cha biashara cha Mahakama Kuu kushughulikia kesi za Biashara ingawa ngazi ya sharti la ubobezi zaid halijafikiwa