Tazama Albamu ya Picha
WAZIRI WA MAMBO YA NJE YA CHINA WANG YI AWASILI CHATO MKOANI GEITA
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Geita Wilayani Chato leo tarehe 07 Januari 2020 na kupokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Chato mkoani Geita leo tarehe 08 Januari 2021
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi mara baada ya kuzungumza na wageni mbalimbali katika hafla fupi ya utiaji saini wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga km 341 kati ya Shirika la Reli Tanzania TRC na Ubia wa Kampuni mbili za Kichina, China Civil Engineering Construction Corporation CCECC na China Railway Construction Corporation Limited CRCC.
Hatimiliki ©2015 Ikulu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha | Kanusho|
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na Inaendeshwa na Ofisi ya Rais Ikulu