Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tovuti Rasmi ya Rais

Wasifu

Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE
Dkt JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa tarehe 7 Oktoba mwaka 1950 Msoga, mkoa wa Pwani, mtoto wa sita katika familia ya watoto tisa. Amemuoa mama Salma Kikwete na wamebarikiwa watoto nane.

 

Kazi

Mwaka 1976 alijiunga na Chuo Kikuu cha Maofisa wa Jeshi Monduli na kutunukiwa Cheo cha Luteni Kanali na baadaye kuwa Mkufunzi Mkuu na Kamisaa wa Siasa katika chuo hicho. Mheshimiwa Kikwete amefanya kazi katika Chama cha Mapinduzi kwa nyadhifa mbalimbali kwenye mikoa ya Singida na Tabora na  wilaya za Nachingwea na Masasi.

Mwaka 1988 aliteuliwa kuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa  Jimbo la Bagamoyo na akateuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Maji, Nishati na Madini. Nyadhifa nyingine alizoshika ni Waziri wa Fedha mwaka 1994 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

Alishika rasmi wadhifa wa urais mwaka  2005 na kuchaguliwa tena 2010 kwa muhula mwingine wa  miaka mitano.

 

Elimu

Alipata elimu ya msingi na ya kati katika shule za Msoga na St. John Bosco Lugoba kati ya mwaka 1958 na 1965. Aidha, alipata elimu ya sekondari katika shule za sekondari za Kibaha (1966 – 1969) na Tanga (1970 – 1971).Alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi, 

 

Nyadhifa nyengine

Chairman of the African Leaders Malaria Alliance (ALMA) for 2010-2011


Chairman of the East African Community (EAC) Jan 2010


Chairman of the African Union (AU) 2008


Co-Chair of the Helsinki Process on Globalisation and Democracy 2004


Chairman of the Council of Ministers of the Southern African Development Community (SADC) 2004


Chairman of the Council of Ministers of the Organisation of African Unity (OAU) 1997


Chairman of the Council of Ministers of the East African Community (EAC) 1997


Chairman of the Board of Governors of the East African Development Bank (EADB ) 1995